Home | Terms & Conditions | Help

April 25, 2024, 9:00 am

NEWS: WAFANYAKAZI 2 WA GAZETI LA MWANANCHI MBARONI KWA UPOTOSHAJI

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni linawashikilia wafanyakazi wawili wa Gazeti la Mwananchi kwa tuhuma za kutuma taarifa za uongo na Uzushi kuhusu ugonjwa wa Corona kwenye Group la WhatsApp.

Watuhumiwa hao ni Haidary Hakam(27) na Alona Tarimo(42) wote ni Maafisa Biasha wa Gazeti hilo.

Taarifa iliyotolewa usiku wa jana May mosi na Kamanda wa Polisi Kinondani SACP Edward Bukombe amesema kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo siku ya Aprili 5, mwaka huu.

Kamanda Bukombe amesema mtuhumiwa wa kwanza Ndugu Haidary Hakim alituma ujumbe kwenye Group la WhatsApp nakuandika "Za chini chini kuna Padre wa Peramiho amefariki na Corona, ametokea Italy kisha akakaa Dar es salaam Kidogo kisha akaele Mbeya kwa kutumia ndege na Baadae akaondoka kwa private kuelekea Songea. Akazidiwa Akawekwa ICU Peramiho sasa amefariki. Waliomuhudumiwa wamemuweka karantine"

Na kosa la mtuhumiwa wa pili Ndugu Alona Tarimo ni kuunga mkono Ujumbe wa ndugu Haidary Hakim katika group hilohilo.

Akiandika "hivi kigogo hajazipa ili aposti theni Serekali waweke wazi"

Kamanda Bukombe ametoa wito kwa watanzania wengine wanaotumia mitandao ya Kijamii kuacha tabia ya kutoa taarifa ambazo hazijadhibitisha na Serekali au mamlaka husika.