Home | Terms & Conditions | Help

May 19, 2024, 12:40 am

CHINA YASITISHA UHUSIANO NA MAREKANI BAADA YA SPIKA PELOSI KWENDA TAIWAN

Utawala wa China umesema leo kuwa umesitisha ushirikiano katika maeneo mengine mengi kiwemo kufuta au kusitisha majadiliano na Marekani kuhusu masuala kadhaa kuanzia mabadiliko ya tabia ya nchi na juhudi za kupambana na madawa ya kulevya, kufutia ziara ya spika wa bunge la Marekani huko Taiwan.

Hatua hizo zinazojiri wakati uhusiano kati ya Washington na Beijing unazidi kuzorota, ndiyo za karibuni zaidi katika mkuroro wa hatua ilizoahidi China kuiadhibu Marekani, kwa kuruhusu ziara ya Nancy Pelosi kwenye kisiwa inachodai kuwa himaya yake.

China ilianzisha luteka kubwa za kijeshi siku ya Alhamisi katika maeneo sita nje kidogo ya pwani ya Taiwan, ambazo imesema zitaendelea hadi Jumapili. Maafisa wamesema makombora yamerushwa juu ya anga la Taiwan, huku China ikisema zaidi ya ndege 100 za kivita na meli 10 za kivita zimeshiriki katika mazoezi hayo ya mashambulizi halisi karibu na Taiwan.

Marekani imelaani luteka hizo na imemuita balozi wa China nchini humo kupinga hatua hiyo, huku China nayo ikiwaita mabalozi wa mataifa ya kundi la G7 kupinga matamshi ya viongozi wa mataifa kuhusu mzozo wa Taiwan.