Home | Terms & Conditions | Help

May 5, 2024, 3:09 pm

NEWS: PPRA YASAINI MKATABA NA UNDP WA BIL.40/-

DODOMA: Mamlaka ya ununuzi wa Umma PPRA imesaini mkataba wa ushirikiano na shirika la mpango wa maendeleo la umoja wa mataifa UNDP wa (Dola milioni 17) zaidi ya billion 40 kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wa PPRA ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wazawa kuchangamkia fursa katika miradi ya maendeleo.


Mkataba huo umesainiwa leo Jumatano April 24, 2024 Jijini Dodoma ambapo afisa Mtendaji mkuu wa PPRA Eliakim Maswi amesema mkataba huo licha ya kurahisisha ununuzi wa vifaa kwa bei nafuu, utawezesha PPRA kutoa elimu kwa wazawa kutumia fursa hiyo iliyoelekezwa kisheria ili kuendelea kuwajengea uwezo wa kuteeleza miradi.

“Kwa sasa ujue ni kitu cha ajabu sana hata mradi mdogo unakuta Wachina wanaunza karanga Kariakoo yaani kweli inaingia akilini haiwezekani ,kwasasa unaweza kukuta mradi mkubwa hata wa bilioni 20 mfano au bilioni 10 unakuta Kampuni inayojenga ni yakichina,”

Amesema kwa Mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma inaelekeza miradi yote ya gharama ya chini ya Bilioni 50 inapaswa kupewa wazawa ila hilo limekua halionekani kwa vitendo kutokana na uelewa Mdogo wa wananchi.

“ Hatuwezi kuwajenga kwa kila kitu kuwapa wageni wajenge hii nchi haijengwi hivyo kwa sababu sheria ya ununuzi imetamka hivyo , sasa tukasema inawezekana watu wetu wanahitaji kujengewa uwezo kwahiyo tumekubaliana watu wetu wajengewe uwezo ili wawe na uwezo wa kusimamia miradi na kufanya wenyewe ,”

“Wafanyabiashara au wakandarasi au Wazabuni wenye uwezo wa kutengeneza miradi hii ya kati na midogo lazima wajengewe uwezo ukisema uwezo ukoje tunatofautiana katika uwezo watu wote hawafananibhata budole byako havilingani sasa inatakiwa watu wote wawezeshwe ili kuwa na uwezo katika kutekeleza miradi hii ,” amesema Maswi

Muwakilishi mkazi wa UNDP Tanzania Shigeki Komatsubara amesema Tanzania imepiga hatua kubwa kufikia uchumi wa kati hivyo shirika hilo litaendelea kutoa ushirikiano ili kuchochra maendeleo.