Home | Terms & Conditions | Help

May 19, 2024, 1:20 am

NEWS: ABASI MTEMVU AWATIMUA TENA NDUGU ZAKE KWENYE NYUMBA YA MAMA YAO

Dar es Salaam. Aliekua Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu ameidharau amri ya Mahakama ya Kituo Jumuishi cha utoaji Haki za Kifamilia (Ndoa, talaka na mirathi) iliyoweka zuio la muda la kutowafukuza ndugu zake Ibrahim Mtemvu na Jasmine Mtemvu kwenye nyumba ya mama yao mzazi iliyopo kitalu namba 1036/2 eneo la Haile Selas, Masaki jijini Dar es salaam.

October 2013 - Kamera Yangu

Mzizi wa sakata hili ni Abbas Mtemvu aliteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi ya Marehemu Mama yao Joyce Kilungo na Mahakama ya Mwanzo, Temeke katika shauri la mirathi namba 474 la mwaka 2017.

Lakini ndugu zake wawili, Ibrahimu Mtemvu na Jasmine Mtemvu walikata rufaa Mahakama ya Wilaya ya Temeke, katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki kuhusu Masuala ya Kifamili (ndoa, talaka na mirathi), Temeke.

Inaelezwa kuwa Mara baada ya Abbas kuwa msimamizi wa Mirathi hiyo anadaiwa kuiuza nyumba hiyo ya familia kwa Mustafa Mohamed, mkurugenzi wa kampuni ya Delligent Group kwa Sh900 milioni na fedha zote akazitafuna peke yake bila kushirikisha ndugu zake.

Lakini Oktoba 4, mahakama ilitoa zuio la muda ili kwa Abass kuwaondoa ndugu zake kwenye nyumba hiyo ya marehemu mama yao hata baada ya kudaiwa kuiuza.

Wakili wa ndugu hao, Adili Kiiza alisema baada ya wateja wake kufukuzwa kwenye nyumba hiyo Oktoba 7, walienda kufungua shauri dogo mbele ya Hakimu Simon Swai kumtaka Abbas ajieleze kwa nini asifungwe kwa kuendelea kudharau amri ya mahakama iliyopanga kusikiliza kesi hiyo Oktoba 17.

Ibrahim alisema mahakama ilitoa zuio kwa waleta maombi na wanufaika na mirathi kutotolewa kwenye nyumba hiyo lakini ndugu yao Abbas amekuwa akiwatumia mabaunsa kuwazuia wasiingie ndani hivyo kukiuka agizo la lililotolewa na mahakama hiyo.