Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 5:13 pm

NEWS: BODI YA MIKOPO HESLB YAWAONGEZEA WANAFUZI BILIONI 84 ZA MIKOPO

Dar es Salaam. Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Tanzania (HESLB) imesema kwamba imeongeza tena shilingi Bilioni 84 kwenye bajeti yake ya mikopo kwa mwaka huu wa masomo 2022/2023 ambayo ni sawa na asilimia 14.7 ikilinganishwa na kiasi kilichotengwa hapo awali.

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru amesema kutokana na ongezeko hilo la fedha kwa sasa bajeti ya mikopo imefikia Sh654 bilioni kutoka Sh570 bilioni iliyotengwa hapo awali ambayo ni sawa na ongezeko la Tsh Bilioni 84.

Government directs HESLB to ensure a smooth disbursement of loans | The Citizen

Kiasi hicho kitawezesha wanafunzi 28,000 kupata mikopo kwa robo ya kwanza ya mwaka wa masomo na tayari fedha hizo zimeshafikishwa katika vyuo husika.

Hadi kufikia leo jumla ya wanafunzi 166,438 wamepangiwa mikopo yenye thamani ya Sh424.5 bilioni kati yao wa mwaka wa kwanza ni 68,460 na wanaoendelea ni 97,978.

Kulingana na Badru wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanaolengwa kunufaika na mikopo hiyo kwa mwaka huu ni 71,000.

“Bajeti isingeongezwa ni wazi wanafunzi 28,000 wangekosa mikopo lakini kutokana na hatua hii iliyochukuliwa wataweza kupata ufadhili huu. Hawa waliopata walikuwa tayari wameshafanyiwa tathmini na kuonekana mahitaji yao ni makubwa,”amesema Badru.