Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 10:04 pm

NEWS: HAITMAYE WAKULIMA WAANZA KUINGIA KWENYE MFUMO WA USAJILI

Serekali imesema kuwa Wizara ya kilimo nchini imeanza utaratibu wa kuwasajili wa Wakulima kwa mwezi mmoja sasa na wamefikia takribani Wakulima Milioni 1.3 kwenye mfumo na karibia 50% wamepata namba zao za siri na namba maalumu (unique identity number).

TFRA | News

Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kupitia ukurasa wake wa Twitter hii leo Jumamosi Octoba 1, 2022

“Mfumo huu tunachukua alama za vidole (biometeic fingers), picha na baadae maeneo (GPS coordinates) ya mashamba, mfumo huu wa ruzuku na TEHAMA (digitization & digitalization) una changamoto zake mf. usambazaji (distribution network) lakini tumedhamiria kukabiliana nazo zote”

Wakulima nchini wahamasishwa kujisajili kwenye mfumo wa ruzuku | Muungwana BLOG


“Tumejiwekea malengo mpaka mwezi December, tuwe tumefikia lengo la kaya milioni 7 kusajiliwa ambazo zitatusaidia kujua taswira pana ya aina ya wakulima na hali ya kilimo nchini”

“Jambo moja linalonitia moyo, Wakulima wengi waliosajiliwa wana utambulisho (NIDA), taswira inaonesha zaidi ya asilimia 70 wana umri wa kati 18-50yrs ,kwamba ile dhana kuwa kilimo kimetawaliwa na Mababu inaonekana kuwa sio sahihi”