Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 6:14 pm

NEWS: HARMONIZE AMDAI ANJELA BILIONI 1

Taarifa za kuaminika zinadai kuwa Msanii wa Bongofleva na Mmiliki wa Lebal ya Konde Music Harmonize anamdai msanii wa lebal yake hiyo Angella kiasi cha Tsh Bilioni 1 ikiwa kama msanii huyo atahitaji kuondoka mwenyewe katika Lebal hiyo.

Kwa mujibu wa mkataba wa Anjella na Konde Music unasema kuwa ikiwa kama lebal yake ya Konde Music itavunja mkataba wake basi msanii huyo atapewa platforms zake zote za mitandao ya kijamii ikiwemo Instagram na Youtube, lakini ikiwa ni Anjella ndiye atakayevunja mkataba huo basi atalazimika kumlipa boss wake Harmonize kiasi cha Shilingi Bilioni 1.

Lakini taarifa zinasema kuwa Lebal hiyo ya Konde Music inaonekana kumuacha mwanadada huyo kimya kimya bila kumtaarifu hatua ambayo imemlazimisha Msanii huyo kwenda Baraza la Sanaa la Taifa BASATA kwa lengo la kupata ufafanuzi wa kisheria na kumlazimisha Harmonize kumpa haki zake za kisheria kwa mujibu wa mkataba wake.

Siku ya Tarehe 1 Novemba BASATA ilimwita Harmonize ofisi kwake kwa lengo la kufanya mazungmzo na msanii huyo ili kujibu madai ya Msanii wake Anjella, lakini taarifa ndani ya BASATA zinadai kuwa Harmonize hakufika na BASATA imempangia tarahe nyingine.

Madai ya Anjela kuachana na lebo hiyo rasmi badala ya ilivyo sasa kimyakimya, yamekuja wiki moja baada ya lebo hiyo kumalizana na wasanii wengine wawili Cheed na Killy, waliokuwa na malalamiko yanayofanana na hayo.

Inadaiwa kuwa bosi huyo wa lebo ya Konde Music kutaka kuachana na Angela ni pamoja na kutorudisha faida ya kile walichowekeza kwake.

Nyota huyo alitambulishwa kwenye lebo hiyo Machi 11, 2021, ambapo aliachia wimbo ‘Kama’ aliomshirikisha Harmonize na mpaka sasa wimbo huo umeshatazamwa zaidi ya mara milioni tatu kwenye mtandao wa Youtube, mwingine ni ‘Sina Bahati’. Nyimbo zilizofanya vizuri kwa kupata watazamaji wengi Youtube ni ‘Nobody’ aliouachia mwaka 2021 uliotazamwa mara milioni nne na ‘Kioo’ aliomshirikisha Harmonize uliotazamwa mara milioni tano.