Home | Terms & Conditions | Help

May 19, 2024, 1:04 am

NEWS: KARANI WA SENSA AJINYONGA

Tabora. Karani wa Sensa aliyefahamika kwa jina la Edmund Zakayo Mkazi wa wilayani Igunga mkoani Tabora, amejinyonga usiku wa kuamkia leo Agosti 23, 2022 kabla ya kuanza kazi ya Sensa, huku akiacha ujumbe kuwa asilaumiwe mtu yeyote kutokana na tukio hilo la Kujinyonga.

Karani huyo ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Buchenjegele sehemu ya ujumbe wake aliouacha amesema kuwa amejinyonga kutokana na matatizo ya kifamilia kwahiyo mtu yoyote asihusishwe huku akiomba kuzikwa katika maeneo ya Skonge mkoani Tabora.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani mara baada ya tukio hilo amesema ipo haja ya Serekali kuanzisha vitengo maalumu vya ushauri (cancealing ) kutokana na kushamiri kwa matatizo hayo.