Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 8:54 pm

NEWS: MAGANDA YA MAYAI YATUMIKA KAMA TIBA YA MIMEA.

DODOMA: Ikiwa tunaendelea na Msimu wa Mvua, Wakulima wameshauriwa kutumia kilimo ikolojia ikiwemo mbegu bora, Mbolea za asili ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi, kutengeneza rutuba ya udogo lengo kumsaidia kuongeza uzalishaji.

Ushauri huo umetolewa katika mkutano wa Wadau wa Kilimo Ikolojia kwa Maisha na maendeleo endelevu’’ ulioandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Action Aid Tanzania uliofanyika Kijiji cha Msanga Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma Novemba 22, 2022.

Akitoa elimu kwa wakulima wenzake Mkulima Magreth Malogo amesema katika kukabiliana na Mabadiliko ya tabia ya nchi wao kama Jukwaa la Vijana Chamwino wameweza kubuni maganda ya Mayai yanayotumika kufukuza vidudu kwenye mimea.

‘’Maganda ya Mayai kama maganda ya mayai unayachukua unayatwanga kwa njia ya kiyenyeji kwenye kinu, au unayafikicha ukishamaliza kuyatwanga unaenda kumwagia kwenye mimea yako, ile Halfu yake inasaidia kuzua wadudu wasumbufu,’’amesema Malogo.

‘’Lakini pia ukiyatwanga utoka na ardhi yetu hii imeathiriwa na mabadiliko ya tabia ya nchi, katika kuirusha ardhi imkae sawa yale maganda ya mayai ukiyatwanga na ukaenda kumwaga shambani kwako inapunguza ACID ya udongo,’’ amesisitiza Malogo.

Mbali na hayo wameendelea kushauri kuboreshwa kwa mashamba darasa , kutenga bajeti ndani ya vyanzo vya mapato ndani ya halmashauri kununua kipimia udongo ili kusaidia kujua afya ya udongo inayotakiwa.

Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri wa Wilaya ya Chamwino Samweli Kaweya amewaasa Wakulima kutumia dhana,mbolea, madawa ya asili , katika suala nzima la kilimo.

Kwa upande wake Ofisa kilimo Chamwino Living Kilawe amesema ‘’Wilaya ya Chamwino imekuwa ikikubwa na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kuwa na joto kali, mvua kutonyesha na ukame wa muda mrefu hivyo tunaendelea na jitihada za kupambana na changamoto hizo,’’

Pia ameendelea kwa kusema Wilaya imegaramia upatikanaji wa hati ya Shamba la Ekari 8000 katika Kijiji cha Membe Ambapo bwawa kubwa la kuvunia maji kwaajili ya shughuli za mifugo na Kilimo ujenzi unaendelea ambapo takriban bilioni 11.96 zitatumika.

Naye Mratibu wa Habari, mawasiliano na teknolojia kutoka Shirika la Action Aid Tema Hassan amesema lengo la kuanda Mkutano huo wa wadau ni kuwakumbusha wananchi wa Wilaya ya Chamwino na Vijiji Vyake juu ya umuhimu wa kilimo ikolojia kuelekea msimu wa kilimo unaokuja 2022/2023 .

‘’Kilimo ikolojia nyezo ya wakulima katika kusaidia kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi, katika Mkoa wa Dodoma kwa Ujumla tunaona kunachangamoto kubwa sana ya mabadiliko ya tabia ya nchi anandicho kilichotufanya kuwa na msukumo na mpango wakuhakikisha elimu hii ya kilimo ikolojia inawafikia ili kurejesha hali ya kilimo na kuwafanya wananchi wawe na maendeleo endelevu,’’amesema Hassan