Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 9:45 pm

NEWS: MALKIA WA UINGEREZA AFARIKI DUNIA

Malkia wa Uingereza Elizabeth II, ambaye amekaa muda mrefu katika Utumishi wake nchini Uingereza, amefariki dunia jioni ya leo akiwa Balmoral akiwa na umri wa miaka 96, baada ya kutawala kwa miaka 70.

Ndugu na Familia yake ilikusanyika katika Jumba lake la Uskoti baada ya wasiwasi kuongezeka juu ya afya yake mapema Alhamisi.

Malkia alishika kiti cha ufalme mnamo 1952 na alishuhudia mabadiliko makubwa ya kijamii.

Kutokana na kifo chake, mwanawe wa kwanza Charles, mwanamfalme wa zamani Wales ataongoza nchi kwa maombolezo kama Mfalme mpya na mkuu wa nchi kwa milki 14 za Jumuiya ya Madola.

Katika taarifa yake, Mfalme alisema: "Kifo cha mama yangu mpendwa Malkia, ni wakati wa huzuni kubwa kwangu na wanafamilia wote.

"Tunaomboleza sana kifo cha Malkia mpendwa na Mama anayependwa sana. Najua kumpoteza ni jambo litakalosikika sana kote nchini, Milki na Jumuiya ya Madola, na kwa watu wengi duniani kote."

Alisema katika kipindi cha maombolezo na mabadiliko yeye na familia yake "watafarijiwa na kudumishwa na ufahamu wetu wa heshima na mapenzi ya kina ambayo Malkia alipewa sana".

Katika taarifa, Jumba la Buckingham lilisema: "Malkia alikufa kwa amani huko Balmoral mchana huu.

"Mfalme na Malkia Consort watasalia Balmoral jioni hii na watarejea London kesho."

Watoto wote wa Malkia walisafiri hadi Balmoral, karibu na Aberdeen, baada ya madaktari kumweka Malkia chini ya uangalizi wa matibabu.

Mjukuu wake, Prince William, pia yuko hapo, pamoja na kaka yake, Prince Harry, njiani.

Muda wa Malkia Elizabeth II kama mkuu wa nchi ulihusisha ukali wa baada ya vita, mabadiliko kutoka kwa himaya hadi Jumuiya ya Madola, mwisho wa Vita Baridi na kuingia kwa Uingereza - na kujiondoa kutoka - Umoja wa Ulaya.

Utawala wake ulihusisha mawaziri wakuu 15 kuanzia na Winston Churchill, aliyezaliwa mwaka 1874, na akiwemo Liz Truss, aliyezaliwa miaka 101 baadaye mwaka wa 1975, na kuteuliwa na Malkia mapema wiki hii.

Alifanya kikao cha kila wiki na waziri mkuu wake katika kipindi chote cha utawala wake.

Katika Jumba la Buckingham huko London, umati wa watu waliokuwa wakisubiri taarifa kuhusu hali ya Malkia walianza kulia waliposikia kifo chake. Bendera ya Muungano juu ya Kasri ilishushwa hadi nusu mlingoti saa 18:30 BST.

Malkia alizaliwa Elizabeth Alexandra Mary Windsor, huko Mayfair, London, tarehe 21 Aprili 1926.

Wachache walitabiri kwamba angekuwa malkia lakini mnamo Desemba 1936 mjomba wake, Edward VIII, alijiondoa kwenye kiti cha ufalme na kuolewa na Mmarekani aliyetalikiana mara mbili, Wallis Simpson.