Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 11:58 pm

NEWS: MFALME ZUMARIDI AKUTWA NA KESI YA KUJIBU

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza leo Octoba 4, 2022 imewakuta na kesi ya kujibu mchungaji maarufu jijini Mwaza Diana Bundala maarufu Zumaridi na wenzake wanane wanaokabiliwa na kesi ya jinai.

CHEKI!! VITUKO vya MFALME ZUMARIDI MAHAKAMANI.../Aonyesha ISHARA mbalimbali Mbele ya MAHAKAMA....... - YouTube


Zumaridi na Wafuasi wake wanane wamekutwa na kesi ya kujibu kwa shtaka la kuwazuia Maafisa wa Serikali kutekeleza majukumu yao pamoja na kuwajeruhi Askari Polisi wawili wakati kuwakamata.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama Monica Ndyekobora ameiahirisha kesi hiyo ambapo itatajwa tena Oct 17 hadi 21, 2022 itakaposikilizwa mfululizo Mawakili wa Utetezi kuleta mashahidi 30, vielelezo visivyopungua 12 ikiwemo video itakayooneshwa Mahakamani hapo

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Diana Bundala maarufu Zumaridi, Neema Julian, Anitha Yesaya, Suzana Saimon, Veronica Emmanuel, Amos Kailembo, Isaya John, Isaka Mafuru na George Maloji wanadaiwa kutenda makosa hayo Feb 23, 2022.