Home | Terms & Conditions | Help

May 19, 2024, 1:20 am

NEWS: MTATURU ASHAURI KUANZISHWA KWA BODI YA ALIZETI.

DODOMA: Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu(CCM) ameshauri kuwepo kwa bodi ya alizeti itakayoweka mikakati maalum ya kuhakikisha zao hilo linalimwa kwa wingi nchini ili kuondokana na uhaba wa mafuta ya kula.

Mtaturu ametoa ushauri huo Februari 10 bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia Mpango wa Kitaifa wa Maendeleo wa mwaka mmoja 2021/2022 na Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2021/2022 hadi 2025/2026.

“Tumeambiwa kuna mikoa nane unaweza kulima alizeti tukiwa na bodi hii ya alizeti tutaweka mkakati maalum wa kuhakikisha kwamba tunalima alizeti kwa wingi tunawezesha viwanda vyetu,"amesema.

Ameshauri kuwepo mkakati na msukumo maalum kwenye kilimo cha alizeti ili kuhakikisha kama kuna bodi ya korosho, pamba,sukari basiiwepo pia ya bodi ya alizeti ili kuwepo msukumo mkubwa zaidi.

Mtaturu amesema licha ya kuwepo zao hilo la kimkakati lakini nchi inaagiza mafuta ya kula nje ya nchi na kwamba kwa mwaka nchi inatakiwa kutumia tani 570,000 za mafuta lakini uwezo wa kuzalisha nchini ni tani 210,000 tu.

“Hii ina maana zaidi ya nusu tunaagiza nje, ina maana tunatumia fedha za kigeni nyingi kuagiza mafuta ya kula, hili jambo ni vyema tukabadilisha mwenendo wetu tukahakikisha kwamba zao la alizeti pamoja na mazao ya mbegu za mafuta tuchukue hatua kubwa kuhakikisha tunawekeza vya kutosha,"amesisitiza.

“Nimeangalia mkakati wa serikali katika kuhakikisha tunakuza kilimo cha umwagiliaji kutoka kwenye heka zilizoelezwa 461,00 na kuongeza kufikia 694,00 bado tuna safari ndefu lazima tuwe na mapinduzi ya kweli ya kuhakikisha tunawekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji