Home | Terms & Conditions | Help

May 19, 2024, 1:41 am

NEWS: MUHINDI RISH SUNAK AMEKUWA WAZIRI MKUU WA UINGEREZA

Aliyekuwa Waziri wa fedha nchini Uingereza, Rishi Sunak, ameteuliwa leo Jumatatu kuwa kiongozi wa chama cha Conservative, na sasa antarajiwa kuchukua uongozi wa nchi hiyo kama waziri mkuu wa Uingereza.

New UK PM Rishi Sunak's Indian Connection Explained In 10 Points

"Rishi Sunak amechaguliwa kuwa kiongozi wa Chama cha Conservative," ametangaza Graham Brady, anayehusika na masuala haya ndani ya chama tawala kwa miaka 12. Akiwa hajakusanya idadi inayohitajika ya uungwaji mkono, Penny Mordaunt alikubali kushindwa, na "kumuunga mkono" Rishi Sunak kwenye Twitter. Kansela huyo wa zamani wa Exchequer, 42, anakuwa kiongozi wa kwanza wa serikali asiye mzungu katika historia ya Uingereza.

Sunak, anakabiliwa na kibarua kizito cha kusuluhisha mgogoro ndani ya chama na wa kiuchumi ambao umeikumba Uingereza.

Anakuwa waziri mkuu wa tatu kuingia madarakani ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, baada ya kujiuzulu kwa Boris Johnson na Liz Truss ambaye alijiuzulu baada ya siku 45 ofisini.

UK PM Contender Rishi Sunak Reveals How He Met Akshata, Opens Up about Fatherhood

Ushindi wa Sunak, umetangazwa baada ya kujiondoa kwa mshindani pekee Penny Mordaunt aliyeshindwa kupata uungwaji mkono wa chama.

Sunak alishindwa na Liz Truss katika uchaguzi wa awali, lakini sasa, chama chake kimeonekana kuwa na imani naye kuliko wagombea wengine, kukabiliana hali ya kudorora kwa uchumi, mfumuko wa bei, na kuongezeka kwa bei ya nshati.

Ameahidi kwamba ataiongoza Uingereza kwa kuzingatia uadilifu, weledi na uwajibikaji. Amewaambia wanasiasa wa upinzani kwamba hakutakuwa na uchaguzi wa mapema kama chama cha Labour kilivyokuwa kimesema.

Sunak, ambaye ni mhindi wa kwanza kuwa waziri mkuu wa Uingereza, na mwenye umri wa chini kabisa wa miaka 42, anasubiri mfalme wa Uingereza Charles wa 3 kumuomba kuunda serikali.