Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 11:07 pm

NEWS: PADRI WA KIKATOLIKI KORTINI KWA KULAWITI WATOTO

Moshi. Padri mmoja wa Kanisa Katoliki katika Jimbo la Moshi, Sostenes Soka ameburuzwa Mahakamani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro kwa tuhuma za udhalilishaji wa kingono wa kulawiti watoto kadhaa wa waumini wake.

Kiongozi huyo wa kiroho, amepandishwa leo Jumatatu, Septemba 26, 2022 kusomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Salome Mshasha.

Padri anadaiwa kulawiti na kubaka watoto zaidi 10 waliokuwa na utaratibu wa kwenda Kanisani kwenye mafunzo ya kidini.

Lakini hata hivyo Hakimu wa kesi hiyo amewazuia waandishi wa habari kuingia katika chumba cha mahakama kwa kile kilichoelezwa ni aina ya kesi inayomkabili padri huyo.