Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 7:09 pm

NEWS: SABABU ZA KISS DANIEL KUSHINDWA KUFANYA SHOW

Waandaaji wa Tamasha la Summer Amplified Str8up Vibes leo wametoa tamko kufuatia Msanii wa Nigeria Kizz Daniel kushindwa kufanya Show kabisa ukumbini usiku wa kuamkia leo Jumatatu Agosti 8,2022 kama ilivyotakiwa na kupelekea Mashabiki kukasirika na kuamua kuvunja vunja vitu vya ukumbini hapo.


Usiku wa jana Msanii huyo Mkali wa wimbo wa Buga alipaswa kufanya show hiyo katika Ukumbi wa Next Door Arena licha ya ukweli kuwa msanii huyo alikuwepo Jijini Dar ea salaam.

Taarifa ya Str8up Vibes leo imesema "Sisi katika Str8up Vibes tunasikitika sana kwa kilichotokea kwenye Tamasha la SUMMER AMPLIFIED Aug 07 2022 ambapo Kizz Daniel hakutumbuiza kama ilivyotarajiwa, tunakubali kwamba hii imesababisha kuvunjika moyo kwa Wateja wetu waaminifu na Wadau muhimu wa muda mrefu waliohusika, tunachukua hatua zinazofaa katika kushughulikia suala hili kwa ukali na kuuhakikishia Umma na mashabiki waliolipa na kuhudhuria kwamba tunafanya kila tuwezalo kuhakikisha tunaweka hali vizuri, tunaomba subira yao tunaposhughulikia hili"

"Str8up Vibes ni kampuni inayoheshimika na iliyojijengea sifa thabiti, kuridhisha Wateja wetu siku zote imekuwa jukumu letu kwa miaka mingi ambayo tumekuwa katika biashara hii, tutawasiliana kwa hatua zaidi zinazofuata, Ahsante kwa kuelewa" - Damian Mapala, Mkuu wa mawasiliano

Lakini kwa mujibu wa marafiki wa karibu wa Kiss Daniel wamesema kuwa sababu kuu ni kwamba Kiss Daniel alisahau nguo za kufanyia Show nchini kwao Nigeria huku sababu ya pili imetwajwa kuwa Kiss Daniel alipata ugonjwa wa tumbo ghafla.