Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 7:45 pm

NEWS: SEREKALI KUJENGA BARABARA YA HARAKA YA KIBAHA MORO YAKULIPIA

Dar es salaam. Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi nchini Prof. Makame Mbarawa amesema Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi nchini inakusudia kupata mkandarasi hivi karibuni atakayejenga barabara ya haraka (express way) kutoka Kibaha mkoani pwani hadi mkoani Morogoro ambayo itakuwa ya kulipia.
Mbarawa Amesema na kwa madereva wasiotaka kulipia watatumia barabara ya kawaida.

Mbarawa ameyasema hayo jana Nov 16,2022 Kwenye Mkutano wa 15 wa mwaka na wadau wa Uchukuzi.

Mbarawa amefafanua kuwa gharama za fedha hizo zitatolewa na mkandarasi mwenyewe na yeye mkandarasi atanufaika kwa kutoza kodi kwenye barabara hiyo.

Mkandarasi huyo anakusudiwa kupatikana mwezi 5 mwakani