Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 10:29 pm

NEWS: SIMBA YAMTIMUA KOCHA WAKE ZORAN MAKI

Dar es salaam. Club ya wekundu wa msimbazi Simba Sports Club leo Septemba 6, 2022 imetangaza kuachana na Kocha wake mkuu Mserbia, Zoran Maki. baada ya makubaliano ya pande zote mbili kuafikiana.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo kupitia kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo ilieleza kusitisha mkataba wake wa mwaka mmoja aliousaini pamoja na kocha wa viungo, Sbai Karim na kocha wa makipa Mohammed Rachid.

Zoran Manojlovic met en garde ses joueurs

Kikosi hicho ambacho kinajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa tatu dhidi ya KMC kesho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kitakuwa chini ya Kocha msaidizi Selemani Matola huku mchakato wa kutafuta Kocha Mkuu ukiendelea.

Katika michezo miwili ambayo Zoran alikiongoza kikosi hicho ameshinda yote akianza na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Geita Gold Agosti 17 kisha ushindi wa 2-0 kutoka kwa Kagera Sugar Agosti 20 yote ikichezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Zoran mwenye uraia pacha wa Serbia na Ureno alitambulishwa rasmi kukinoa kikosi hicho Juni 28 mwaka huu akichukua mikoba ya Mhispania Pablo Franco aliyejiunga nayo Novemba 10, 2021 kabla ya kutimuliwa Mei 31, 2022.