Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 8:54 pm

NEWS: TUZO ZA UBORA KITAIFA ZANZINDULIWA

DODOMA; Tuzo za Ubora wa kitaifa kwa mwaka 2022/ 2023 Zimezinduliwa leo Oktoba 27, 2022 na wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara, kwa kushirikiana na Shirika la Viwango Tanzania TBS na sekta binafsi.


Akizindua tuzo hizo Kaimu Katibu Mkuu wizara ya uwekezaji ,Viwanda na biashara Aristides Mbwasi amesema mashindano ya tuzo hizo yamegawanywa katika vipengele vitano ambavyo Tuzo kwa kampuni ya mwaka , Tuzo kwa bidhaa ya ubora ya mwaka ,tuzo kwa huduma bora ya mwaka ,tuzo kwa Muuzaji bora wa bidha nje ya nchi na tuzo ya mwisho ni Mtu mmoja aliyefanya vizuri kwenye masuala ya ubora.“kwa kipengele cha kwanza hadi cha nne zimeandaliwa tuzo kwenye makundi mawili kwa kila kipengele yani tuzo kwa kampuni kubwa na pia tuzo kwa wajasiriamali wadogo wadogo wakati( SME) na kipengele cha tano kinahusisha tuzo kwa mmoja pekee,”amesema Mbwasi

Mkurugenzi mkuu Shirika la viwango Tanzania TBS Dkt Yusuph Ngenya amesema kuwa washiriki wa tuzo za ubora za SADC wanapaswa watokane na washindi wa tuzo za ubora za kitaifa.

“ Tuzo hizi ni sehemu mipango ya serikali katika kuboresha huduma na bidhaa zinzotengenezwa nchini kupitia matumizi ya viwango na kanuni za ubora kwa taasisi za umma na sekta binafsi ,”amesema

Hata hivyo ameendelea kwa kusema “ Lengo ni kuhakikisha kuwa Mifumo ,bidhaa na huduma zinakidhi ubora kitaifa ,kikanda na kimataifa na hivyo kufanya vizuri kwenye masoko ya ngazi zote,” amesema Dkt Ngenya.

Naye Mwakilishi kutoka ZBS Hafsa All Salimu Mkurugenzi wa Idara ya maendeleo ya viwango akimwakilisha mkurugenzi wa shirika la viwango ZBS amesema kwa upande wa Zanzibar wameshiriki na wanatarajia kutoa uelewa kwa wafanyabishara na wajasiriamali washiriki kwa wingi.

Tuzo za ubora zilianzishwa ikiwa ni makubaliano baina ya wanachama wa jumuiya ya maendeleo kwa nchi za kusini mwa Afrika (SADC)ili kutambua na kukuza sekta ya biashara kupitia ubora wa bidhaa .