Home | Terms & Conditions | Help

May 19, 2024, 12:04 am

NEWS: URUSI UMEKICHUKUWA RASMI KIWANDA CHA NYUKLIA CHA UKRAINE

Calls for restraint as attacks continue near Ukraine power plant | Nuclear Energy News | Al Jazeera

Hatimaye Urusi imetwaa rasmi kituo cha nyuklia cha Zaporizhia kusini mwa Ukraine, ambacho imekikalia kijeshi kwa miezi kadhaa, kulingana na agizo liliotiwa saini na Rais wa nchi hiyo Vladimir Putin jana Jumatano, Oktoba 5.

"Serikali italazimika kuhakikisha kuwa vifaa vya nyuklia vya kituo hiki(...) vinakubaliwa kuwa mali ya shirikisho", agizo hilo, lililochapishwa na Urusi.

Russia accused of kidnapping head of Ukraine nuclear plant | Russia-Ukraine war News | Al Jazeera

Kituo cha nyuklia cha Zaporizhia, kilicho karibu na jiji la Enerhodar, mnamo Agosti 4, 2022.Tangazo hilo limetolewa siku chache kabla ya kiongozi wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA), Rafael Grossi, akijianda kufanya ziara nchini Ukraine na Urusi.

Kutolewa kwa agizo hili kunakuja wakati ambapo taarifa za magharibi zinadai kuwa majeshi ya Urusi yanazidi kupoteza vitani nchini Ukraine katika maeneo yalinyakuliwa kinyume cha sheria huko Donetsk, Luhansk, Kherson na Zaporizhia.

Kwa mujibu wa ramani ya kijeshi iliyochapishwa na Wizara ya Ulinzi ya Urusi siku ya Jumanne, jeshi la Urusi limerudi nyuma takriban kilomita 30 katika eneo la Kherson kusini mwa nchi hiyo. Kremlin imeahidi Jumatano kwamba "maeneo haya yatarudishwa".

Ukraine inaendelea kukabiliana na mashambulizi yake. Ukraine imedai kusonga mbele katika eneo la Luhansk mashariki, ambalo kufikia sasa linadhibitiwa kabisa na jeshi la Urusi. "Sasa ni rasmi. Uvamizi wa eneo la Luhansk umeanza. Maeneo kadhaa tayari yamekombolewa kutoka mikononi mwa jeshi la Urusi," gavana wa Ukraine wa eneo hilo, Sergiï Gaïdaï, amesema Jumatano.

Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya zimekubaliana kuhusu vikwazo vipya dhidi ya Moscow. Uamuzi huu unakuja baada ya kunyakuliwa na Urusi ya maeneo manne ya Ukraine. Makubaliano hayo yalihitimishwa katika ngazi ya mabalozi wa nchi Ishirini na Saba. Majina na vyombo vinavyolengwa na vikwazo hivi vipya vitachapishwa katika Jarida Rasmi la EU siku ya Alhamisi, wanadiplomasia wamesema. Vikwazo hivyo hasa vinaadhibu uagizaji kutoka Urusi wa bidhaa za kimkakati na kupunguza bei ya mafuta ya Urusi.