Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 11:28 pm

NEWS: VODACOM YAPATA BOSS MPYA KUTOKA MTN AFRICA

Dar es Salaam. Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Group imemteua Philip Basiimire kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vodacom Tanzania Plc atakayeanza kuhudumu katika kazi hiyo Mwezi Octoba mwaka huu.

Bw. Basiimire ambaye ni raia wa Afrika kusini anakuwa mtu watatu kuteuliwa na kampuni hiyo ndani ya kipindi miezi 10.

Novemba Mosi, 2021 Hisham Hendi alitangaza kujiuzulu rasmi nafasi hiyo baada ya kuitumikia kwa miaka mitano kabla ya Sitholizwe Mdlalose.

Mdlalose aliyepata uteuzi Vodacom Group Afrika Kusini alidumu siku 310 katika ofisi hiyo kabla ya kutangazwa Philip anayeanza kutumiaji nafasi hiyo wiki mbili zijazo.

Hata hivyo, kabla ya kutangazwa Philip, kampuni hiyo ilikuwa chini ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Hilda Bujiku aliyedumu kwa takribani miezi mitatu yenye chachu katika mageuzi ya kidigitali.

Aliifanya kuwa kampuni ya kwanza kutumia huduma za Hologram chini ya masafa ya intaneti ya 5G.

“Philip Besiimire ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Vodacom Tanzania kuanzia Oktoba 15 mwaka huu. Amejiunga na kampuni hii kutokea MTN Afrika kusini alikokuwa Mkuu wa masoko, usambazaji na uendeshaji wa kikanda tangu mwaka 2019,”imenukuu sehemu ya taarifa ya Vodacom.

“Amewahi kufanya mbalimbali akiwa MTN ikiwamo Mtendaji wa shughuli za Kikanda nchini Afrika Kusini, Ofisa Mtendaji Mkuu Sudan kusini, Ofisa Mkuu wa masoko Zambia, Ofisa Mkuu wa Masoko na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu Eswatini.”

Kampuni ya Vodacom Tanzania kwa mujibu wa wa Repoti ya mwezi Juni mwaka huu ina wateja milioni 17.2 wa huduma za simu ikifuatiwa na milioni 15.2 wa kampuni ya Airtel Tanzania na milioni 14.9 wa Kampuni ya Tigo Tanzania