Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 11:07 pm

NEWS: VYUMBA VYA FARAGHA, NDOA ZA UTOTO BADO KIZUNGUMKUTI CHAMWINO.

CHAMWINO: Wanafunzi wa Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma wameendelea kulia ukosefu wa nyumba vya Faragha , vifaa Kama Taulo za kike ,hali hiyo hupelekea ongezeko la utoro kwa watoto wa kike pindi wanapokuwa katika siku zao .


Pia changamoto ya ndoa za utoto ,imeonekana hutokea mara kwa mara ndani ya Wilaya hiyo kutokana kinachodaiwa umaskini au Ugumu wa maisha ,tamaa za wazazi ,pamoja na mila na desturi potofu ambazo hupelekea watoto kuozeshwa wakiwa na umri mdogo nakukatisha ndoto zao.

Hata hivyo serikali na wadau wengine wamekuwa na jitihada mbalimbali za pamoja za kuhakikisha wanamaliza tatizo hilo lakini bado kumekuwepo na changamoto ya mazingira ya siyo rafiki ya kujifunzia ikiwemo ya nyumba vya Faragha,vifaa Kama Taulo za kike.


Wakizungumza katika Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa kike Duniani yalioandaliwa na shirika lisilo la kiserikali ACTION AID TANZANIA ikishirikiana na , DEO, Jeshi la Polisi, wadau wa Elimu, Dawati la Jinsia, maadhimisho yaliyofanyika Oktoba 15, 2022 Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.


Akiongea katika Maadhimisho hayo Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Mlowa Barabarani Irene Rameck amesema ikiwa imetokea ameichafua hali hiyo hupelekea kujibagua kwa kuwa anakwepa aibu kwa wanafunzi wenzake.

Mwanaisha Juma ni Mwanafunzi kutoka shule ya Sekondari Msanga amesema ili kutatua changamoto hizo marekebisho ya sheria ya ndoa kandamizi dhidi ya watoto wa kike yafanyike, elimu itolewe kwa jamii kuhusu Afya ya uzazi na jamii kuacha mila na desturi zinazowakandamiza watoto wa kike.


Naye Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo OCD Wilaya ya Chamwino Grace Salia amesema ili kutatua changamoto ya ndoa za utotoni jamii iendelee kupaza sauti ili kupambana na changamoto hiyo huku akizitaka Asasi zingine kuendelea kusaidia ujenzi wa vyumba vya faragha na taulo za kike '’Haki na Wajibu vinaenda Pamoja niwatake watoto kuwaheshimu wazazi /walezi ili kutimiza ndoto zenu,’’.