Home | Terms & Conditions | Help

May 19, 2024, 1:20 am

NEWS: WAMAREKANI WAADHIMISHA MASHAMBULIZI YA SEPTEMBA 11

Rais wa Marekani Bw. Joe Biden wa ameadhimisha kumbukumbu ya miaka 21 tangu mashambulizi ya kigaidi nchini humo ya Septemba 11, 2001 kwa kuweka shada ya maua kwenye jengo la wizara ya ulinzi.

Maadhimisho hayo yanafanyika baada ya kama mwaka mmoja tangu Biden alipohitimisha operesheni ya muda mrefu na ya gharama kubwa ya kijeshi nchini Afghanistan, ambayo Marekani na washirika wake waliianzisha katika kupambana na ugaidi.

Msemaji wa Baraza la Usalama wa Taifa John Kirby amesema hotuba ya Biden itatambua athari za mashambulizi hayo ya 2001 nchini humo na ulimwengu kwa ujumla pamoja na kuwakumbuka karibu watu 3,000 waliouwawa siku hiyo, baada ya watekaji wa al-Qaeda kuzidhibiti ndege za kibiashara na kuziangusha kwenye majengo ya Kituo cha kibiashara cha Kimataifa, wizara ya ulinzi na uwanja wa ndege wa Pennysylvania.