Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 11:28 pm

NEWS: WEMASEPETU "SINA TATIZO NA DIAMOND, SISI NIWASHIKAJI" "

Dar es Salaam. Miss Tanzania wa mwaka 2006, Wema Abraham Sepetu amesema Staa wa Muziki Nchini Tanzania Diamond Platnumz ni rafiki yake na watu wasitafsiri tofauti wanapoona hajawahi kuwa na urafiki katika mtandao wa kijamii wa Instagram.

Wema ameeleza hayo jana Ijumaa Februari 21, 2020 wakati akiingia makubaliano na kiwanda cha rasta cha rasta cha Angel kuwa balozi wa bidhaa zao.

Wema amesema suala la ‘kutomfollow’ Diamond katika mtandao huo ni makubaliano yao tangu walipokuwa na mahusiano.

Kuhusu uhusiano wake na mkali huyo wa Bongofleva, Wema amesema hawana ugomvi wowote, “kuna wakati hata tulitaka kuwa na kipindi katika televisheni ya Wasafi. Kipindi ambacho tungefanya kwa kushirikiana mimi, Anti Ezekiel na Zamaradi Mketema, lakini yakatokea ya kutokea kikayeyuka.”

“Kama mnavyoona sasa, mimi nina App yangu ya Wema na Zamaradi ana TV yake kila mtu anatengeza vipindi vyake huko.”

Pia wema alitolea maelezo swala la Kupunguza uzito wake kutoka 109 hadi 55

Huu mwili ndio niliokuwa nauhitaji, wakati ninashinda taji la Miss Tanzania mwaka 2006 nilikuwa na kilo 55. Kwa kilo zile 109 nilikokuwa naelekea si kuzuri.”

"Nitajitahidi nibaki na wembamba huu kwa kuwa unanipa amani, wembamba raha jamani asikuambie mtu," amesema Wema.

Mlimbwende huyo amesema wapo wanaohusisha wembamba wake na ugonjwa, “siwajali kwani hata nilivyokuwa mnene niliitwa majina mengi kama tembo, nyumba nakadhalika.”