Home | Terms & Conditions | Help

May 19, 2024, 1:41 am

NEWS: ZITTO AMWAGIA SIFA RAIS SAMIA KIGOMA

Kigoma. Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe amemwamgia sifa kedekede Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM taifa Samia Suluhu Hassan kwa kusema kuwa hali ya kisiasa nchini imekuwa ya utulivu sana na kwamba hali hiyo ya utulivu inasaidia kuchochea shughuli za maendeleo nchini.

Kauli hiyo za Zitto ameitoa hii leo Oktoba 18, 2022 wakati akitoa salamu zake kwa mgeni wao Rais Samia katika Ziara yake ya Kikazi Mkoani Kigoma, Zitto amesema njia ya kujenga maridhiano ya kitaifa ndio njia pekee itakayoifanya nchi isonge mbele.

Zitto amesema makala aliyoandika Rais Samia Suluhu Hassan ya Julai 1 siku ya kuadhimisha miaka 30 ya mfumo wa vyama vingi alielezea falsafa yake ya R4 kwaajili ya kuliweka taifa pamoja na kulijenga,hivyo aanamuomba Rais aweze kuendeleza hizo za mageuzi ya kisiasa.

“Nachukua nafasi hii kukupongeza Rais Samia kwa juhudi za kuwaweka Watanzania pamoja bila kujali itikadi zao.

“Uwepo wangu hapa ni ishara kuwa haiangalii vyama vya siasa vya watu bali unawaangalia watanzania kwa pamoja,” amesema Zitto Kabwe

Zitto amesema Rais Samia anaweza kujenga miundombinu yakiwemo madaraja, barabara, viwanja vya ndege na bandari, lakini Watanzania watamkumbuka kwa mawazo aliyoyaonisha katika Makala yake hiyo yenye dhamira ya kuwaleta Watanzania pamoja.

Adiha amesema chama chake wanatarajia kuwasilisha uchambuzi na mapendezo yao kuhusiana na muswada uliowasilishwa bungeni wa Bima ya Afya kwa Wote, hivyo ameomba Serikali yake ipokee mawazo yao na kuyafanyia kazi.

“Sisi kama chama cha upinzani tumefanya uchambuzi wetu na tutawasilisha mapendekezo yao ya kuboresha muswada huo, tunaomba Serikali yako ipokee na itafakari ushauri wetu,” amesema.