Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 7:45 pm

SEREKALI: KUKATIKA KATIKA KWA UMEME KWISHA MWEZI DESEMBA

Serikali imesema kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu wanatarajia kuwa tatizo la umeme la kukatika katika litakwisha mara baada ya mradi wa umeme wa Kinyerezi 1 Extension utatoa megawati 185 kukamilika.

ZamaMpya TV on Twitter: "Naibu Waziri wa Nishati Wakili Stephen Byabato amesema kuwa mradi kabambe wa kupeleka umeme kwenye vijiji unaitwa REA three round two unaendelea nchi nzima na mkoa wa Mara

Kauli hiyo ya Serekali imetolewa hii leo Novemba 2, 2022, Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato, wakati akitoa ufafanuzi kufuatia changamoto ya ukatikaji wa umeme inayoendelea nchini.

"Tunayo changamoto kidogo ya upungufu wa vyanzo vya uzalishaji wa umeme hasa kwenye maji, hilo limepelekea baadhi ya maeneo kukatika umeme au kupewa umeme kwa vipindi tofauti , serikali imeji-commit kabla ya mwezi unaokuja kuisha mradi wetu wa Kinyerezi 1 Extension utakaotupatia megawati 185 umekamilika ili kuondoa matatizo ya kukatika katika umeme," amesema Naibu Waziri Byabato

Shirika la Umeme (Tanesco) lilitoa taarifa tarehe 30 mwezi 11 mwaka huu kuwa ukame unaoikabili nchi ndiyo sababu kubwa ya changamoto ya ukatikaji wa umeme wa mara kwa mara unaoendelea nchini.

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Shirika hilo, Martin Mwambene alisema mabwawa ya kuzalisha umeme ya Hale, Kihansi, Nyumba ya Mungu na Pangani yenye uwezo wa kuzalisha megawati 266 za umeme sasa yanazalisha megawati

Mwambene alieleza kwamba ili kutatua changamoto hii, shirika limechukua hatua ya kujenga njia mpya kutoka kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Luguruni jijini Dar es Salaam ili kuhudumia maeneo yote hadi Chalinze, ili kutoa nafasi ya umeme mwingine kufika katika mikoa hiyo.

“Hii itasaidia kupunguza mzigo wa umeme katika njia ya sasa inayotoka Ubungo hadi Chalinze na hivyo kuruhusu umeme mwingi kwenda katika mikoa tajwa,”

Kujenga njia mpya kutoka kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Lemugrul kilichopo Kisongo jijini Arusha.

“Hatua hii itapunguza mzigo wa umeme unaopita kwenye kituo cha Njiro hivyo kuongeza kiasi kingine cha umeme kufika mikoa ya Kilimanjaro na Tanga,”