Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 8:30 pm

VIONGOZI WA SEREKALI GEITA WATAPELIWA NA MAAFISA IKULU FAKE

Geita. Jeshi la Polisi Mkoani Geita linawashikilia watu watatu kwa waliojifanya maafisa kutoka IKULU kwa kuwatapeli Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi Halmashari na Wakuu wa Taasisi za serikali wakiwadanganya kuwa Rais ameridhishwa na utendaji kazi wao hivyo wanapaswa kutuma pesa ili kupata nafasi za juu.

"Watu ambao tunawashikilia ni Emmanuel John(38) ,Mfipa George (34) na Mussa Nassoro (35), wakati tunawapekua tumewakuta na Simu nyingi pamoja na laini ambazo zina majina ya viongozi wakubwa waandamizi serikalini" Henry Mwaibambe Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita.

"Emmanuel John yeye amekuwa akijitambulisha kama Naibu Katibu mkuu ofisi ya Rais, watu hawa wamekuwa wakiwapigia na kuwasiliana na viongozi mbali mbali na kutoa sifa kuonyesha Rais anaridhishwa na utendaji wao wa kazi" Henry Mwaibambe Rpc Geita.