Home | Terms & Conditions | Help

May 3, 2024, 2:23 pm

NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA

Thamani ya Shilingi ya Kenya, imeporomoka pakubwa dhidi ya dola ya Marekani na kufikia kiwango ambacho kimsingi hakijawahi kushuhudiwa katika historia ya kuundwa kwa Kenya, inaripoti Gazeti la Business Daily.

Helpless Kenya Shilling now at 134 against US dollar in the market

Walioathirika zaidi na kuporomoka kwa shilingi hiyo ni watumiaji wake ambao wanalipia gharama kubwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje.

Kwa mujibu wa gazeti hilo Benki kadhaa za biashara zinauza dola za Kimarekani zaidi ya Sh150 jijini Nairobi, zikizidisha shinikizo kwa shilingi ya Kenya huku zikiweka wateja wake ongezeko jipya la bei inayotokana na sarafu katika bidhaa zinazoagizwa kutoka nje zikiwemo mbolea, vifaa vya elektroniki na magari.

Kenyan shilling hits a new all-time low against the dollar | The Citizen

Wastani wa bei ya dola katika benki kadhaa jijini Nairobi na mashirika matatu ya biashara ya kubadilisha fedha yaliyotolewa na gazeti la Business Daily ilikuwa inaelekea Sh150.

Benki Kuu ya Kenya (CBK), hata hivyo, iliweka wastani wa kiwango cha ubadilishaji kuwa Sh142.98, ikionyesha tofauti kubwa kati ya kiwango rasmi na biashara halisi kama ilivyonukuliwa na wafanyabiashara wa fedha.